Tuesday, September 8, 2015

Nyumba ya ndoto yako: Namna ya kueleza mawazo yako kwa (Architect) Msanifu Majengo

Linapokuja suala la kupata ramani ya nyumba ya ndoto yako, wengi hushindwa kujua wapi pa kuanzia na namna gani ya kupata ramani. Hivyo huishia kushindwa kueleza mawazo yao kwa architect au kunakili ramani nyingine na hivyo kukosa kile wanachokitaka. Unaweza kuvutiwa na design fulani ya nyumba au mchoro lakini unashindwa namna ya kueleza mawazo yako kwa architect.
  Zifuatazo ni dondoo ambazo zitakusaidia kueleza mawazo yako mpya au ukarabati kwa architect:

1. Fanya maamuzi ni nini hasa unachotaka na ndoto zako ni realistic ziko ktk uwezo wako.

2. Kuwa na mawazo yako binafsi kwanza kabla ya kukutana na architect.
Hii ni sawa na pale unapoenda saluni au kwa fundi nguo, ni muhim kwanza kuwa na your favourite style, fashion na vitu unavyovipenda. Hii itakusaidia kuongea lugha moja na architect na kuelewana. Ktk ulimwengu huu wa utandawazi, ni rahisi kuyaelezea mawazo yako vizuri zaidi kwa architect kwa kuwa na mkusanyiko wa picha za nyumba, rangi, staili, materials, furniture nk unazozipenda(inspirations). Mfano facebookpage kama "Ujenzi Zone", application ya simu inayoitwa "Houzz" nk hii humwezesha architect wako kubadilisha ndoto zako kuwa nyumba inayoonekana.

3. Jadiliana na architect wako ili kujua kama ana uwezo kuleta ndoto zako kwenye uhalisia. Unaweza pia kuomba akuonyeshe kazi zake za zamani alizowahi fanya. Pia unaweza kujadiliana na architect wako juu ya design ya nyumba yako kadiri anavyendelea kuandaa michoro ya nyumba yako.

4.Fikiria mapema bajeti ya nyumba ya ndoto yako. Kabla ya kukutana na msanifu majengo kuwa na rough picha ya gharama za nyumba yako mpaka kukamilika. Hii itamwezesha architect wako kujua mipaka yako na kudesign nyumba ambayo itakuwa ndani ya bajeti yako.

5. Mweleze architect wako juu ya plans zako za sasa na za badae ili aweze kuyaweka mawazo yako katika design. Mfano ikiwa unataka ghorofa na unajua badae utashindwa kupanda ngazi kwenda kwenye master bedroom yako iliyoko ghorofa ya kwanza, unaweza kumwambia architect wako adesign one bedroom kwenye ground floor yenye quality ya masterbedroom.

6. Mwamini architect wako kuwa ana best design intensions.
Wakati wewe unajali zaidi juu ya mwenekano mzuri na bajeti, architect hufikiria mengi zaidi ya hayo ikiwa ni pamoja na uimara, usalama nk. Architect atasikiliza mawazo yako na mwisho wa siku atakuja na kitu kilicho bora kwa ajili ya nyumba ya ndoto yako.

7.Kama kuna sehemu/ kitu hajaelewa kuwa huru kumwuliza ama kumchallenge architect wako.
Jinsi maelezo yako yatakavyokuwa clear ndivyo design ya nyumba yako nayo itakuwa vile utakavyo. Wengi huogopa kuwatumia architect, engineer wataalamu wengine kwa kuhofia gharama zao au kuwa na mtazamo hasi juu ya wataalamu hawa, lakini ukweli utabaki kuwa "rahisi ni ghali zaidi".

Ukiwa utahitaji huduma ya usanifu majengo usisite kuwasiliana nasi kwa namba hizi.
0755 571604, 0715 799 402 na 0783 095 169
Best luck on your dream house!

Saturday, September 5, 2015

NAMNA BORA YA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI.

NAMNA BORA YA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI.
Umiliki wa nyumba ni miongoni mwa ndoto za walio wengi wetu, kila mtu ana shauku ya kumiliki nyumba yake mwenyewe. Shauku hii inatimia pale tu mtu anaponunua au kujenga nyumba hiyo (achilia mbali njia nyingine za upataji aseti hii). Hata hivyo, tulio wegi tunaogopa kuanza mchakato wa ujenzi kwa kudhani kuwa gharama za ujenzi ni kubwa mno. Ukweli ni kwamba: Kukosekana kwa taarifa muhimu zinazohusu ujenzi kunatufanya tujenge bila kujua kwa undani tunachokifanya matokeo yake gharama zinakuwa kubwa maana mambo mengi hufanyika aidha bila kupanga au kwa kuona wengine wamefanya.

GHARAMA ZA UJENZI  ZINAWEZA KUATHIRIWA NA MAMBO YAFUATAYO:
1. Mbinu za ujenzi zinazotumika (construction techniques).
Kiwango cha utaalamu/teknolojia kinachotumika katika ujenzi chaweza kuongeza au kupunguza gharama za ujenzi. Mara nyingi watu huamua kutumia njia fulani kwa sababu tu pengine waliona mahali imetumika, hata hivyo, ukifikiria zaidi waweza kutumia njia nyingine ambayo ni nafuu zaid katika ujenzi(inayoweza kufanywa hata na mafundi wa kawaida na wakiwa wachache) na ikaleta ubora ule ule (au zaidi).

2. Upatikanaji wa vifaa vya ujenzi.
Vifaa vya ujenzi vitapaswa vinunuliwe / vipatikane eneo lililokaribu na mahali ambapo nyumba itajengwa. Hii itapunguza gharama za usafirishaji pia itatwezesha kukamilisha kazi ndani ya muda mfupi.

3. Uimara wa vifaa hivyo.
Vifaa vyote vya ujenzi havina budi kuwa imara na madhubuti. Hii itapunguza gharama za baadae za ukarabati (maintainance cost). Na hivyo kuokoa fedha ambazo zinaweza kutumika kwa shughuli zingine za maendeleo.

4. Uandaaji wa vifaa vya ujenzi kabla na wakati wa kujenga
Uaandaaji wa vifaa vya ujenzi unapaswa uzingatie kwamba hauachi mabaki mengi (ambayo yatatupwa). Ikiwa fundi anakatkata matofali bila taratib maalumu, kuna uwezekano wa kuwa na vipande vingi ambavyo havitatumika na mwisho wake vitatupwa.

5. Usanifu wa jengo lenyewe.
Kwa kawaida gharama za ujenzi ni mchakato (zinaanza nyumba inapojengwa na zinaendelea kadri nyumba inavyotumika). Hivyo basi, msanifu majengo (architect). Anaweza kusababisha nyumba iwe ya gharama kubwa au ndogo bila kuathiri ubora. Kwa mfano mpangilio wa vyoo ndani ya nyumba kunaweza kupelekea kuwa na bomba nyingi zaidi au chache zaidi (plumbing length).

6. Matumizi ya nishati ndani ya nyumba(power/energy consumption)
Kama ilivyoelezwa katika namba tano hapo juu. Usanifu wa jengo unawea ukapelekea kukawa na matumizi makubwa au kidogo ya nishati. Kwa mfano msanifu anaweza kusanifu jengo ambalo halitahitaji matumizi ya lazima ya feni na viyoyozi.

7. Hali ya eneo ambapo nyumba inaenda kujengwa.(site condition)
Hali ya site inaweza kupelekea gharama kuwa kubwa au ndogo, hii hutokana na ukweli kwamba site inaweza kuhitaji aina Fulani ya ujenzi ambayo ni ghali kidogo au inahitaji wafanyakazi wengi au watu maalumu wa taaluma Fulani. Kwa mfano kama site ina mteremko mkali. Inaweza kuhitaji aidha ujenzi wa vyumba vya chini (basements) au kuutoa mteremko huo kwa kusawazisha eneo hilo (levelling).

Kama utahitaji huduma zetu za usanifu majengo usisite kuwasiliana nasi kwenye 0755 571604 au 0715 799 402. Tumelenga kwenye kuielimisha jamii yetu kwanza juu ya usanifu majengo.
Best luck on your dream home!

Little things matters alot on house finishing.




Little things matters alot on house finishing.
Katika finishing za nyumba unayoweza kufanya,"Mouldings" zinaweza kutumika kuboresha na kuimarisha mwonekano wa madirisha, milango na kuta. Kuweka "mouldings" kwenye nyumba yako si tu huleta uzuri fulani lakini pia hutoa mwonekano sawa na kuficha nyufa.

Mouldings ni nini?
Ni mapambo ambayo hupendeza kwa macho na zinapofungwa huongeza sifa za tofauti kwenye chumba, milango pamoja na madirisha.

Faida za mouldings ni zipi?
Hutumika kutengeneza mwendelezo(transition) wa kuvutia pale ambapo nyuso mbalimbali zinapokutana.Hutumika kwa madhumuni kuficha migongo ambapo dirisha au mlango hukutana ukuta.Mouldings pia hutumika kuleta mwendelezo mzuri kati ya sakafu au dari na ukuta.

Mouldings zinaweza kuwekwa ktk makundi kadhaa kutokana na jinsi zinavyotumika ktk chumba, juu ya sakafu, kuta, milango, madirisha ikiwa ni pamoja na dari.
"Base Moldings" kimsingi huwekwa sehemu ya chini ya ukuta ambapo inakuja katika kukutana na sakafu.
"Chair rails" ni moulding ambayo  huweka kwa ukuta, karibia na usawa wa urefu wa mgongo wa kiti.Kazi yake hasa ni kukinga kuta kuharibiwa na viti
wakati viti ni vinapovutwa nyuma.
"Casings" aina ya moldings ambayo hukusudiwa kufanya milango na madirisha kuonekana kwa urahisi zaidi.
"Crown moulding" ni moulding ambayo huwekwa juu ya ukuta, ambapo ukuta na dari zinakutana pamoja. Pia hutumikia kuficha pembe inayofanywa kati ya kuta na dari.

Mouldings huweza kutengenezwa kwa materials ya mbao,  gypusum,  plaster nk. Uchaguzi wa rangi ya mouldings na kuta au nyuso nyingine ni jambo la kuzingatia sana. Pia zipo mmouldings za ndani na za nje. Aidha urembo wa namna hii kwenye nyumba nyingi ni nadra sana kuuona na kuzifanya nyumba nyingi kuonekana kawaida tuu.

Nini maoni yako juu ya aina hii ya finishing ktk nyumba? Kama umependa mada hii like na ushare na mwingine.

Kwa ushauri na maelezo zaidi kuhusiana na usanifu majengo tembelea tena page hii.