Saturday, September 5, 2015

NAMNA BORA YA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI.

NAMNA BORA YA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI.
Umiliki wa nyumba ni miongoni mwa ndoto za walio wengi wetu, kila mtu ana shauku ya kumiliki nyumba yake mwenyewe. Shauku hii inatimia pale tu mtu anaponunua au kujenga nyumba hiyo (achilia mbali njia nyingine za upataji aseti hii). Hata hivyo, tulio wegi tunaogopa kuanza mchakato wa ujenzi kwa kudhani kuwa gharama za ujenzi ni kubwa mno. Ukweli ni kwamba: Kukosekana kwa taarifa muhimu zinazohusu ujenzi kunatufanya tujenge bila kujua kwa undani tunachokifanya matokeo yake gharama zinakuwa kubwa maana mambo mengi hufanyika aidha bila kupanga au kwa kuona wengine wamefanya.

GHARAMA ZA UJENZI  ZINAWEZA KUATHIRIWA NA MAMBO YAFUATAYO:
1. Mbinu za ujenzi zinazotumika (construction techniques).
Kiwango cha utaalamu/teknolojia kinachotumika katika ujenzi chaweza kuongeza au kupunguza gharama za ujenzi. Mara nyingi watu huamua kutumia njia fulani kwa sababu tu pengine waliona mahali imetumika, hata hivyo, ukifikiria zaidi waweza kutumia njia nyingine ambayo ni nafuu zaid katika ujenzi(inayoweza kufanywa hata na mafundi wa kawaida na wakiwa wachache) na ikaleta ubora ule ule (au zaidi).

2. Upatikanaji wa vifaa vya ujenzi.
Vifaa vya ujenzi vitapaswa vinunuliwe / vipatikane eneo lililokaribu na mahali ambapo nyumba itajengwa. Hii itapunguza gharama za usafirishaji pia itatwezesha kukamilisha kazi ndani ya muda mfupi.

3. Uimara wa vifaa hivyo.
Vifaa vyote vya ujenzi havina budi kuwa imara na madhubuti. Hii itapunguza gharama za baadae za ukarabati (maintainance cost). Na hivyo kuokoa fedha ambazo zinaweza kutumika kwa shughuli zingine za maendeleo.

4. Uandaaji wa vifaa vya ujenzi kabla na wakati wa kujenga
Uaandaaji wa vifaa vya ujenzi unapaswa uzingatie kwamba hauachi mabaki mengi (ambayo yatatupwa). Ikiwa fundi anakatkata matofali bila taratib maalumu, kuna uwezekano wa kuwa na vipande vingi ambavyo havitatumika na mwisho wake vitatupwa.

5. Usanifu wa jengo lenyewe.
Kwa kawaida gharama za ujenzi ni mchakato (zinaanza nyumba inapojengwa na zinaendelea kadri nyumba inavyotumika). Hivyo basi, msanifu majengo (architect). Anaweza kusababisha nyumba iwe ya gharama kubwa au ndogo bila kuathiri ubora. Kwa mfano mpangilio wa vyoo ndani ya nyumba kunaweza kupelekea kuwa na bomba nyingi zaidi au chache zaidi (plumbing length).

6. Matumizi ya nishati ndani ya nyumba(power/energy consumption)
Kama ilivyoelezwa katika namba tano hapo juu. Usanifu wa jengo unawea ukapelekea kukawa na matumizi makubwa au kidogo ya nishati. Kwa mfano msanifu anaweza kusanifu jengo ambalo halitahitaji matumizi ya lazima ya feni na viyoyozi.

7. Hali ya eneo ambapo nyumba inaenda kujengwa.(site condition)
Hali ya site inaweza kupelekea gharama kuwa kubwa au ndogo, hii hutokana na ukweli kwamba site inaweza kuhitaji aina Fulani ya ujenzi ambayo ni ghali kidogo au inahitaji wafanyakazi wengi au watu maalumu wa taaluma Fulani. Kwa mfano kama site ina mteremko mkali. Inaweza kuhitaji aidha ujenzi wa vyumba vya chini (basements) au kuutoa mteremko huo kwa kusawazisha eneo hilo (levelling).

Kama utahitaji huduma zetu za usanifu majengo usisite kuwasiliana nasi kwenye 0755 571604 au 0715 799 402. Tumelenga kwenye kuielimisha jamii yetu kwanza juu ya usanifu majengo.
Best luck on your dream home!

No comments:

Post a Comment