Saturday, November 28, 2015

3D Modelling: Hurahisisha mawasiliano na uwasilishaji wa mradi wako

3D Modelling ni sehemu mojawapo katika huduma za kudesign na ujenzi wa majengo.3D modelling humsaidia mteja kujenga taswira hasa jinsi jengo lake itakavyokuwa baada ya kujengwa. Aidha hutumika kwa ajili ya kuonyesha mwonekano wa jengo mpya, ukarabati mpya, mwonekano wa ndani na wa nje.3D hutokana na vipimo halisi vya design ya jengo na huwa katika uwiano fulani na jengo halisi. Pia huweza kuonyesha aina ya materials na rangi halisi katika jengo.

Watu wanaweza kuona ugumu kupata taswira ya jengo likiwa kwenye 2D. Faida za 3D Modelling ni pamoja na kuweza kuzungusha jengo katika kompyuta na kuliona jengo katika pembe tofauti na nyakati tofauti za siku kama mchana na usiku. Hivyo ni rahisi kulibadilisha jengo katika hatua ya designing kuliko wakati wa kujenga ambapo huwa gharama zaidi na wakati mwingine kushindikana.

Je ni sababu gani za msingi za kutumia 3D Modelling?
Kuongeza Soko:-Katika miradi 3D Modelling hurahishisha uwasilishaji wa mawazo kwa mwekezaji kwa sababu ya uhalisia wa rangi, vivuli, vitu na material katika jengo. Macho huvutiwa na picha hizi zaidi na hivyo thamani ya jengo/mradi huongezeka.

Katika Zabuni:- 3D hurahisisha kazi kueleweka vizuri na kwa urahisi zaidi na hivyo kuweza kufanyiwa marekebisho kwa urahisi zaidi. Hivyo mteja huwa na uhakika wa mwonekano wa mwisho wa jengo ambalo anaenda kuwekeza.

Kurahisisha mawasiliano:- Hata wateja ambao hawana ujuzi juu ya usanifu majengo na hawaelewi alama au mpangilio fulani, kwa kutumia picha za 3D huweza kuelewa vyote na kuelewana kati ya pande mbili.
Animation:- Hizi ni 3d sinema ambazo huonyesha mienendo ya watu, magari, jua na vitu vingine vinavyohusiana na jengo na hivyo kulipa uhai zaidi.

Architects and Community tunatoa huduma ya 3D Modelling yenye uhalisia wa kweli zaidi na ubora wa hali ya juu. Nini maoni yako juu ya mada hii?