Friday, April 1, 2016

Nani alisema nyumba ndogo haziwezi kuwa nzuri ama kupendeza?

Nani alisema nyumba ndogo haziwezi kuwa nzuri ama kupendeza?


Ukiwa unazunguka sehemu tofauti za jiji mathalani la Dar es Salaam utaona nyumba nyingi mbaya ambazo ungeweza kusema hazistahili kuwa ndani ya jiji. Asilimia kubwa ya nyumba hizi ni ndogo na nyingi zinamilikiwa na watu wa kipato cha chini.
Mwonekano wa baadhi ya nyumba katika jiji la Dar es Salaam

Kuwa na nyumba ndogo kwa kiasi cha kipato chako haimaanishi nyumba yako haistahili kuwa nzuri yenye kuvutia. Sio mara zote unapotaka nyumba ndogo(simple) kwamba wewe ni duni, Kitu unachohitaji ni ubunifu na taarifa(Information).

Unaweza kuwa na nyumba ndogo nzuri yenye kuvutia bila ya kutumia fedha nyingi. Leo hii soko la ujenzi lina vifaa na materils tofauti kwa bei tofauti ambavyo vinaweza kutumika kwenye nyuso za nyumba na kuifanya nyumba yako kuwa na mwonekano wa kupendeza. Vyote vinategemea mapendekezo yako na bajeti yako. Pia uamuzi, kutafuta taarifa, kujua faida na hasara, gharama na matokeo ya vifaa/material tofauti ni mambo yanayohitajika ili kujenga nyumba ya kuvutia pasipo kutumia fedha nyingi.
Uchaguzi sahihi wa material na namna ya kuyatumia huleta mwonekano mzuri
Sio vitu(vifaa/material ya ujenzi) vyote vyenye gharama kubwa vitafanya nyumba yako kuwa na mwonekano mzuri. Vipo vitu vyenye gharama ndogo vinavyoweza kuipa nyumba yako mwonekano mzuri wa kuvutuia.

Faida kubwa ya kuwa na nyumba yenye mwonekano mzuri wa kuvutia hata kama ni ndogo ni kuongezeka kwa thamani ya nyumba yako na pia kuvutia.

Nyumba ndogo za vyumba 1-2 zimekuwa ndio chaguo kubwa kwa wale wanaotafuta sehemu mpya ya kuishi aidha kwa kujenga ama kupanga hasa kwa wale wanaoanza maisha. Nyumba ndogo nzuri ni muhimu kuwa na sebule, sehemu ya kulia, jiko, bafu na vyumba vya kulala. Ngoja tuone nyumba ndogo nzuri, simple zenye kuvutia zinazoweza kujengwa kwa gharama ndogo. Hizi zinaweza kukuhamasisha na kubadilisha mtazamo wako.

Nyumba ndogo, simple na nzuri ni ile yenye mahitaji yote ya msingi.

Ni style ipi unaipenda? Ni material yapi na rangi zipi zinazokuvutia, jua vipaumbele vyako kwanza kisha mtafute mbunifu majengo aiweke ndoto yako kwenye uhalisia.

Contermporary design sio lazima iwe ghorofa na sio kwa wenye hela tu. Ni uamuzi, kuwa na taarifa sahihi na ubunifu

Nyumba iliyokwisha kujengwa inaweza kukarabatiwa na kuwa na mwonekano wa kuvutia kama hii. 
Simple garden itaifanya nyumba yako kuvutia hata kama kiwanja chako ni kidogo.


Unaweza kujenga nyumba ndogo simple yenye mwonekano mzuri kwa kutumia materials zinazopatikana kwenye mazingira yako kwa urahisi, material yenye gharama ndogo za ukarabati, na zisihitaji ufundi mkubwa katika kujenga.

Kwenye makala inayofuata tutazungumzia jinsi ya kufanya nyuso za nyumba yako pamoja na mazingira yawe ya kuvutia kwa gharama nafuu. Tupe maoni yako na share na watu wengine pia ukihitaji huduma za ubunifu na usanifu majengo wasiliana nasi kwa namba hizi: 0755571604 na 0715 799402.